Saturday, January 05, 2013

Azam bila Kipre Tchetche kuivaa miembeni

Timu ya Azam FC katika mchezo wa leo dhidi ya Miembeni FC itamkosa mshambuliaji wake Tchetche Kiprealiyeumia kifundo cha mguu.

Mchezaji huyo aliumia wakati timu yake ikipambana na Coastal Union kwenye mchezo wa juzi wa Kombe laMapinduzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
Kipre aliumia katika dakika ya 24 na nafasi yake ikachukuliwa na mshambuliaji mpya Brian Umony kutoka Uganda,mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu.

Mbali na Tchetche Azam FC pia itaendelea kukosa huduma za Abdulhalim Humud anayemalizia matibabu yake jijiniDSM, John Bocco aliyeko India, na Waziri Salum aliyeumia kidole

Akizungumzia kukosekana kwa wachezaji hao katika mchezo wa kesho kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hallamesikitishwa na tukio hilo na kusema atawatumia wanya mchezaji waliopo kuziba nafasi hiyo ili kupata ushindi.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu itakuwa ikitafuta nafasi ya kusonga mbele, tumefanyamaandalizi ya kutosha kuhakikisha hatupotezi ubingwa na hatupotayari kupoteza mchezo wowote.

Stewart alisemambali na kukosa mchezaji huyo, timu inakabiliwa na majeruhi wengine wawili ambao ni WaziriSalumu aliyeumia kidole cha mwisho na mshambuliaji hatari John Bocco alieyoko nchini India kwa matibabu baadaya kuumia katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Azam FC itacheza mchezo huo wa pili katika Kundi A ambapo timu hiyo inapointi moja sawa na Coastal Union,Miembeni wakiongoza kundi kwa kuwa na pointi 3 huku Mtibwa Sugar wakishika mkia kwa kutokuwa na pointi.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed