Saturday, January 05, 2013

LEWIS HOLTBY ATUA TOTTENHAM HOTSPURS


On the move: Germany midfielder Lewis Holtby is in Qatar on a winter training camp with Schalke
LEWIS HOLTBY KIUNGO WA UJERUMANI AKIWA UWANJANI KATIKA MOZOEZI YA TIMU YA SCHALKE 04

LEWIS HOLTBY AKIWA MAZOEZINI
Skills: Holtby is one of the hottest properties in European football
AKIONYESHA UFUNDI WAKE
Tottenham hotspurs imewapiku liverpool, Arsenal na Everton katika mbio za kumsajili kiungo mchezeshaji wa klabu ya Schalke 04 ya ujerumani Lewis Holtby.

Holtby ambaye ni kapteni wa timu ya taifa ya ujerumani chini ya umri wa miaka 21atajiunga na klabu ya Tottenham endapo atafaulu vipimo vya afya yake na anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi ya uingereza.

Sportsmail imethibitisha kusajiliwa kwa mchezaji huyo ambaye atakuwa akilipwa kitita cha paundi milioni 3.5 kwa mwaka pamoja na ada ya uhamisho ya paundi 530,000.
Mpango huo wa kujiunga na Tottenham umekamilishwa wiki hii baada ya uongozi wa timu ya tottenham kukutana na wawakilishi wa mchezaji huyo katika jiji la Qatar ambapo timu ya Schalke 04 ilikuwa imeweka kambi kwa ajili ya mazoezi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa alipanga kuwaambia marafiki zake kuhusu kuondoka kwake kwenda katika jiji la London siku ya jana lakini taarifa zake zilivuja mapema baada ya klabu ya Tottenham kutangaza kwamba imeshinda vita ya kumsajili mchezaji huyo.

TAARIFA YA KLABU ILISOMEKA HIVI, NANUKUU :Tuna furaha kutangaza kuwa tumefikia makubaliano na nahodha wa ujerumani chini ya miaka 21 Lewis Holtby kujiunga na klabu hii ifikapo mwezi wa julai 2013 kutoka katika klabu ya schalke 04 ya ujerumani inayoshiriki ligi kuu ya ujerumani maarufu kama Bundesliga endapo atafaulu vipimo vya afya yake.

JE NI NANI HUYU LEWIS HOLTBY?
Holtby alizaliwa katika jiji la Erkelenz, karibu na jiji la Dusseldorf na Cologne, nchini ujerumani kwa baba kutoka uingereza na mama wa kijerumani.Kutokana na utaifa wa baba yake Holtby aliruhusiwa kuchezea timu ya taifa ya uingereza mpaka alipochaguliwa rasmi kuwa kapteni wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 21 walipopambana na timu ya taifa ya Azerbaijan 
mwaka 2011

Holtby aliichezea timu ya taifa ya ujerumani chini ya miaka 20 katika kombe la dunia la mwaka 2009 kabla ya kuchaguliwa kuwa kapteni wa timu ya taifa ya ujerumani chini ya umri wa miaka 21.

Alisajiliwa kuichezea Schalke mnamo mwaka 2009 akitokea katika klabu ya Alemannia Aachen ya nchini ujerumani,lakini siku za karibuni ilijulikana kwamba asingeweza kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya ujerumani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akihusishwa na kuhamia klabu ya Arsenal,liverpool na Everton za nchini uingereza kabla ya Tottenham kushinda vita hiyo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed