
David villa yupo tayari kuiomba klabu yake ya sasa ya Barcelona iweze kumwachia ajiunge na klabu ya Arsenal ya uingereza katika dirisha la usajili la januari mwaka huu.
Sportsmail limefichua nia ya Arsene wenger ya kumhitaji mchezaji huyo ambaye anachezea timu ya taifa ya Uhispania katika nafasi ya kiungo wa kati na imethibisha kwamba mipango ya kumnyakua mchezaji huyo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sasa.
Taarifa za ndani zinasema kwamba villa yupo tayari kwenda kukipiga katika klabu ya Arsenal ya uingereza katika dirisha la usajili la januari na anataka kufanya mazungumzo ya kina na klabu hiyo ya jijini London
Inasemekana Villa ana mpango wa kufanya maongezi rasmi na uongozi wa Barcelona ili kuharakisha mipango yake ya kuondoka klabuni hapo, Barcelona imekataa maombi kutoka klabu mbalimbali za ulaya zikimtaka mchezaji huyo kwa mkopo wa muda mfupi na wao wapo tayari kwa mkataba muda mrefu.
Timu ya soka ya Barcelona imewaambia Arsenal inahitaji kiasi cha paundi milioni 16 iweze kumwachia mchezaji huyo lakini inasubiri maombi rasmi ili kuweza kumwachia mchezaji huyo.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ana kiasi cha paundi milioni 70 ambazo anatazamiwa kuzitumia katika usajili wa dirisha dogo la januari na hiyo itamfanya kocha huyo aweze kufanya usajili wa haraka baada ya kushuhudia wachezaji wake wawili wakiondoka Marouane chamach aliyejiunga na klabu ya westham na Johan Djourou anayetimkia klabu ya Hannover
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed