Nigeria imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuilaza Ethiopia kwa bao moja kwa bila katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Victor Moses aliifungia Nigeria bao mbili kunako dakika ya 79, na 90 kwa njia ya penalti.
Sasay Bancha alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa wa Nigeria na hivyo kumlazimisha refa wa mechi hiyo kuumpa kadi ya pili ya njano.
Sawa na ilivyokuwa awali Victor Moses ndiye aliyetunukiwa jukumu hilo la kuupiga penalti na bila kukosea, akafunga la pili na kuhakikisha kuwa Nigeria inasonga mbele kwenye robo fainali ya mashindano hayo.
Super Eagles ilitoka sare mechi zake za kwanza mbili na hivyo ilihitaji shari ushindi mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi ijayo yab mashindano hayo.

No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed