
Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika
Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo wametupwa nje ya mashindano hayo baada ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Burkina Faso ilianza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi tu.
Traore amefunga magoli matatu yakiwemo mawili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne bila.
Dakika chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda ya kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofungana bao lolote.
Katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi zao zligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikigawana ponti moja kila moja na hivyo Burkina Faso kusonga mbele baada yakupata jumla ya pointi tano nayo zambia ikipata pointi mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama moja.
Kabla ya mechi hiyo Zambia ilikuwa na alama mbili na ilihitaji ushindi katika mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi inafuata sawa na Nigeria.
Hata hivyo mabingwa hao watetezi watajialaumu baada ya kukosa nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Collins Mbesuma na Rainford Kalaba hawakuonyesha mchezo mzuri kama iliyotarajiwa na uamuzi wa kocha mkuu wa kumuacha nje nahodha wa Chipolopolo huenda ukashutumiwa vikali, na mashabiki wa Zambia.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed