
Timu ya soka ya Arsenal wiki hii imefanya maendeleo mazuri katika sakata lake la kumbakiza mchezaji wake mahili theo walcott kwa kutoa offa ya paundi milioni 25 kwa mwaka katika mkataba mpya wa mchezaji huyo ili kuondoa utata uliokuwepo kwenye mkataba wake wa sasa.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya uingereza anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano ambapo ataweza kujikusanyia kibunda cha paundi 88,000 kwa wiki pamoja na bonasi ya paundi milioni 3 ya kukubali kuongeza mkataba.
Gazeti la sportsmail la uingereza limethibitisha kuwepo kwa mipango hiyo katika klabu ya Arsenal ya kumbakiza mchezaji huyo kwa miaka mitano ijayo na kwamba mchezaji huyo yupo tayari kujitia kitanzi katika klabu hiyo kwa muda mrefu.
Theo walcott mwenye umri wa miaka 23 sasa aligoma kusaini mkataba mpya wenye gharama ya paundi 75,000 kwa wiki na ivyo kuweka mashakani uwezekano wake wa kuendelea kubaki katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed