Saturday, February 09, 2013

KAGERA SUGAR WAKIJIFUA KWA AJILI YA MCHEZO WAO WA LEO HII NA MGAMBO SHOOTING VPL KWENYE UWANJA WA KAITABA STADIUM, MWAMUZI AMON PAUL KUTOKA MUSOMA KUCHEZESHA MTANANGE HUO.

Wachezaji wa Kagera Sugar wakijifua kwenye uwanja wa Kaitaba Stadium.
Baada ya Kagera Sugar kupoteza Michezo milwili sasa wanajipanga upya kuikabili Mgambo Shooting leo kwenye Uwanja wa Nyumbani Kaitaba Stadium Kuikaribisha Mgambo Shooting, Mchezo utakaochezwa Leo tarehe 9.02.2013. Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Amon Paul kutoka Musoma mkoani Mara. 
Kocha wa Kagera Sugar akicheki wachezaji wake wakijifua kwenye mazoezi
Mgambo Shooting kazi mnayooooo...Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 inaingia raundi ya 16 leo (Februari 9 mwaka huu) kwa mechi nne ambapo Oljoro JKT itaikaribisha Simba jijini Arusha. Mechi hiyo namba 129 itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar. Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 tu utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mgambo Shooting. 
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifanya mazoezi
PICHA ZOTE KWA HISANI YA:http://www.bukobasports.com

1 comment:

only comments that are benefial for this blog is allowed