Monday, February 25, 2013

RYAN GIGGS AFIKISHA MICHEZO 999 KATIKA SOKA

RYAN GIIGGS AKIIFUNGIA MANCHESTER UNITED GOLI DHIDI YA QPR
RYAN GIGGS
Wakati Mkongwe Ryan Giggs akiifungia Manchester United bao la pili katika pambano la juzi la ushindi wa bao 2-0 dhidi ya QPR alikuwa anatimiza idadi ya michezo 999 katika mapambano yote ambayo ameshiriki hii inajumlisha mapambano ya kimataifa na yale ya klabu yake ya Manchester united 

Kwa sasa haifahamiki ni medali ngapi ambazo amekusanya katika maisha yake ya soka hii ni katika mashindano yote ya ligi ya uingereza, kombe la klabu bingwa barani ulaya, kombe la F.A pamoja na lile kombe la ligi maarufu kwa sasa kama Capital one. 

Mchezo wa 1,000 kwa mchezaji huyo utakamilika siku ya jumamosi wakati Manchester united itakopokuwa katika dimba la nyumbani la Oldtrafford kuwakaribisha Norwich, imefahamika kwamba wakati Ryan Giggs akianza kuichezea Manchester united baadhi ya wachezaji wengine walikuwa bado hawajazaliwa. 

Ryan Giggs alianza kuitumikia klabu ya mcnchester united tarehe 2/03/ 1991 katika mechi ambayo Manchester ilipata kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Everton.

Kama mambo yakienda sawa mchezaji huyo akifikisha mapambano 1,000 msimu huu ataingia moja kwa moja katika kundi la magwiji wa zamani ambao wamewahi kucheza mapambano 1,000 katika ligi ya uingereza, wachezaji hao ni Tony Ford na Graham Alexander.

Umri wa  Ryan Giggs tangu ajiunge manchester tarehe 2 March 1991

Paul Scholes, 16 years, four months                            Anderson, two years, 11 months
Rio Ferdinand, 12 years, four months                         Javier Hernandez, two years, eight months
Michael Carrick, nine years, eight months                   Alexander Buttner, two years, one month
Nemanja Vidic, nine years, five months                        Shinji Kagawa, one year, 11 months
Patrice Evra, nine years, two months                           Tom Cleverley, one year, seven months
Robin van Persie, seven years, seven months           Chris Smalling, one year, four months
Darren Fletcher, seven years, one month                   Ben Amos, 11 months
Anders Lindegaard, six years, 11 months                   Rafael, nine months
Ashley Young, five years, eight months                       David de Gea, three months
Antonio Valencia, five years, seven months                Danny Welbeck, three months
Wayne Rooney, five years, five months                        Phil Jones, not born (D.O.B 21 Feb 1992)
Nani, four years, four months                                        Nick Powell, not born (D.O.B 23 Mar 1994)
Jonny Evans, four years two months

ORODHA WA WACHEZAJI WALIOFANIKIWA KUCHEZA MICHEZO 1,000 NA KLABU ZAO
Peter Shilton
Ray Clemence
Pat Jennings
David Seaman
Tony Ford
Graham Alexander

ORODHA YA WACHEZAJI NA MICHEZO WALIOCHEZA KATIKA LIGI YA UINGEREZA
Ryan Giggs (999), Alan Shearer (797), Thierry Henry (773), Dennis Bergkamp (743), Patrick Vieira (728), Tony Adams (735), Steven Gerrard (722), Roy Keane (715), John Terry (664), Eric Cantona (453)

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed