Wednesday, March 13, 2013

BARCELONA YAITANDIKA AC MILAN BILA HURUMA YAIVURUMISHA BAO 4-0(AGGR 4-2) KATIKA UWANJA WA NYUMBANI WA CAMP NOU NA KUFANIKIWA KUTINGA ROBO FAINALI



LIONEL MESSI AKIPIGA MPIRA MBELE YA MABEKI WATATU WA AC MILAN NA KUIANDIKIA BARCELONA BAO LA KWANZA
LIONEL MESSI AKISHANGILIA BAO LA KWANZA LA BARCELONA
MESSI AKISHANGILIA
GERALD PIQUE AKISHANGILIA GOLI LA BARCELONA
ABBIAT AKIOKOA HATARI LANGONI KWAKE
MESSI AKIWA AMEZUNGUKWA NA MABEKI WA AC MILAN
MESSI AKIFUNGA BAO LA PILI LA BARCELONA
XAVI AKIRUKA JUU KUSHANGILIA
KAZI NI KAZI
DAVID VILA AKIIFUNGIA BARCELONA BAO LA TATU
VILA AKISHANGILIA BAO LA TATU
KOCHA MSAIDIZI WA BARCELONA JORDI ROURA AKIWAANGALIA VIJANA WAKE WAKIIANGAMIZA AC MILAN
WACHEZAJI WA BARCELOA WAKISHANGILIA USHINDI WA BAO 4-0
Timu ya soka ya Barcelona jana usiku ilifanikiwa kujikatia tiketi ya kutinga katika 8 bora baada ya kuirarua bila huruma timu ya Ac milan ya italia kwa mabao 4-0 katika uwanja wa nyumbani wa Camp nou.

Iliwachukua dakika 5 Barcelona kuweza kujipatia bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake mahili Lionel messi alipoweza kufunga bao la kwanza kwa umaridadi mkubwa baada ya kupiga mpira mbele ya mabeki watatu wa Ac milan.

Ilionekana kama Ac milan wameamka kutoka usingizini baada ya bao hilo lakini juhudi zao zilivunjwa moyo na Lionel messi tena baada ya kuipatia Barcelona bao la 2 katika dakika ya 40 ya mchezo na hivyo kufanya timu hizo ziende mapumziko uku Barcelona ikwa mbele kwa magoli 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana uku Ac milan wakijaribu kutafuta bao lakini jitihada zao hazikuweza kuzaa matunda baada ya safu ya ulinzi ya Barcelona ikiongozwa na Gerald pique kuweza kusimama imara na kudhibiti mashambulizi yote.

Dakika ya 50 David Vila alizidi kuongeza machungu katika jeraha la Ac milan baada ya kuweza kuipatia bao la tatu na hivyo kuzidi kuwaweka roho juu wapinzani wao ambao walizidi kuhangaika kujaribu kutafuta angalau goli la ugenini bila mafaniko.

Karamu ya magoli ya Barcelona ilikamilishwa na Jordi Alba ambaye aliipatia Barcelona bao la 4 katika dakika ya 90 ya mchezo na hivyo kuiwezesha barcelona kutoka nje wakiwa kifua mbele kwa magoli 4-0.

Kwa matokeo hayo Barcelona inaungana na Real madrid , Borussia Dortmund,Galatasaray,Juventus na Paris St Germain ambazo zimefuzu kwa hatua ya Robo fainali uku matokeo ya mechi mbili zilizobaki yakisubiriwa kwa hamu leo kati ya Bayern Munich au Arsenal na Malaga au Porto

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed