
Klabu ya soka ya Sunderland imempa nafasi mlinzi wa Timu ya Taifa ya Zambia Stopila Sunzu kuweza kufanya majaribi katika klabu hiyo.
Stopila mwenye miaka 23 sasa ni mchezaji wa klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo na ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2015 lakini klabu hiyo imemruhusu mchezaji huyo kuweza kufanya majaribio na klabu hiyo yenye jina la utani ''Black Cats''
Kocha wa klabu ya Sunderland Martin O'Neil amesema kwamba mchezaji huyo alikuwa na maumivu ya mguu yalijomfanya kutolewa nje kabla hajawasili kwa majaribo katika klabu ya Sunderland.
Maumivu hayo yatamfanya mchezaji huyo kukaa nje kwa wiki moja lakini tutaangalia maendeleo yake atakapoanza kucheza.
Awali mchezaji huyo alikuwa asajiliwe na klabu ya Reading mwezi januari 2013,lakini mipango yake haikwenda vizuri kutokana na migongano iliyopo katika mkataba wake na klabu ya TP Mazambe
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed