
Ben Watson akishangilia baada ya kuifungia wigan bao la ushindi dhidi ya man city

Watson akikimbia katika uwanja wa Wembley baada ya ushindi

Watson akiwa amelaliwa na wachezaji wa Wigan

Joe Hart akiruka bila mafanikio kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Watson

Mlinzi wa city Matija Nastasic akionekana kuchanganyikiwa baada ya kipigo

Wachezaji wa Manchester city wakiwa hawaamini baada ya kukosa kikombe cha FA

Mfungaji wa goli la wigan Watson akiwa na kocha Martinez wakinyanyua kikombe cha FA

Kocha wa Wigan Roberto Martinez akiwa na mmiliki wa klabu ya Wigan Dave Whelan wakiinua ndoo ya F.A


Timu ya soka ya Wigan jana imefanikiwa kutwaa kikombe cha F.A baada ya kupata ushindi wa lala salama wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu ya manchester city katika pambano la fainali lililopigwa katika uwanja wa wembley.
Pambano lilikuwa gumu uku kila timu ikijaribu kutumia mbinu nyingi kuweza kuibuka na ushindi katika pambano hilo lakini mambo yalikuwa magumu kwa timu zote kushindwa kufungana.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa timu zote kushindwa kufungana na kilipoanza kipindi cha pili mambo yalizidi kuendelea kuwa magumu kwa timu hizo kushindwa kufungana.
Makocha wa timu zote mbili walijaribu kutumia mbinu zao ikiwa pamoja na kufanya mabadilo kwa timu zao, Kocha wa manchester city Roberto manchini alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Barry (Dzeko 90), Nasri (Milner 54), Aguero, Tevez (Rodwell 69) wakati kocha Roberto Martinez wa Wigan alifanya mabadiliko katika dakika ya 81kwa kumtoa Gomez na nafasi yake kuchukuliwa na Watson.
Dakika ya 84 Manchester city ilishuhudia mlinzi wake Pablo Zabaleta akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha mchezo mbaya.
Pambano liliendelea mpaka dakika ya 90 uku mashabiki wa timu zote wakiamini pambano litakwisha bila kufungana ndipo mchezaji aliyeingia katika dakika ya 81 Watson alipoweza kuifungia timu yake ya wigan kwa goli safi la kichwa katika dakika ya 91 ya mchezo na hivyo kuifanya wigan kuwa bingwa mpya wa kikombe cha F.A
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed