Monday, June 10, 2013

NAMPALYS MENDY MBIONI KUTUA MANCHESTER UNITED

 Nampalys Mendy (Kulia) anayefananishwa na  Claude Makelele
Mendy (Kulia) akiwa katika harakati zake uwanjani

Manchester united wako mbioni kumsajili kiungo machachari wa timu ya Monaco 
Nampalys Mendy. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa ameishtua klabu yake ya monaco baada ya kuweka bayana kwamba anataka kuihama klabu hiyo akiwa mchezaji huru(Free transfer) katika dirisha la usajiri la majira ya joto.

Mendy ambaye uchezaji wake wa soka unafananishwa na kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya ufaransa na klabu ya real madrid Claude Makelele amekuwa mhimili muhimu katika safu ya kiungo ya monaco ambayo inanolewa na kocha Claudio Ranieri na ameweza kuleta mchango mkubwa kwa klabu hiyo kuweza kurejea ligi ya kwanza ya nchini ufaransa.

Akimwongelea mchezaji huyo kocha wa klabu ya Monaco Claudio Ranieri amesema sifahamu vizuri kuhusu tabia yake, mara ya kwanza nilipomwona akicheza mpira nilisema huyu ni Claude Makelele mpya. Nilimwamini na kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara, nashangaa ameamua kuondoka katika klabu hii wakati klabu inamwitaji na hipo tayari kumpa mkataba mpya.

Ameamua kumsikiliza kaka yake pamoja na wakala wake na siyo kocha wake hii ni aibu alimalizia kusema Ranieri.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya ufaransa chini ya miaka 21 amezivutia timu za Nice ya ufaransa lakini yupo mbioni kuongea na klabu ya Manchester united kuangalia uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed