Saturday, June 08, 2013

SERENA WILLIAMS AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA WAZI YA UFARANSA


SERENA WILLIAMS (KULIA) AKIWA NA KOMBE LA USHINDI WA MASHINDANO YA WAZI YA UFARANSA
MAPUMZIKO BAADA YA KAZI NGUMU
MARIA SHARAPOVA AKIRUDISHA MPIRA ULIOPIGWA NA SERENA
BAADA YA PAMBANO SERENA AKIPONGEZWA NA SHARAPOVA
SERENA AKISHANGILIA BAADA YA USHINDI
SERENA AKIPAMBANA NA SHARAPOVA

Mchezaji anayeshikilia nambari moja duniani kwa kina dada Serena Williams, ameshinda kombe  la pili la mashindano ya mashindano ya wazi ya ufaransa ikiwa ni miaka kumi na moja baada ya kushinda tuzo hilo kwa mara ya kwanza.

Serena Williams alimshinda bingwa mtetezi wa mashindano hayo Maria Sharapova wa Urussi kwa seti mbili kwa moja za 6-4,6-4.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na moja kutoka Marekani alitumia muda wa saa moja na dakika arobaini na sita kumpiku mpinzani wake.

Ushindi huo ni wa kumi na sita kwa mchezaji huyo katika mashindano ya tennis ya Grand Slam na anakaribia kuifikia rekodi iliyowekwa na Martina Navratilova na Chris Evert ambao wameshinda mataji kumi na nane kila mmoja.

Serena ambaye hajashindwa katika mashindano thelathini na moja yaliyopita, wengi wanahisi kuwa ana nafasi nzuri sana ya kushinda taji lingine mwezi ujao wakati wa mashindano ya Wimbledon.

Kabla ya fainali hiyo Sharapova, alikuwa amehaidi kuwa atafanya kila juhudi kumshinda mchezaji huyo kutoka Marekani baada ya juhudi zake za kumuangusha katika mashindano kumi na mawili yaliyopita kushindikana.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed