WACHEZAJI WAKISALIMIANA KABLA YA PAMBANO KUANZA
THOMAS ULIMWENGU AKISUMBUA LANGONI MWA IVORY COAST
AMRI KIEMBA AKIWAPITA WACHEZAJI WA IVORY COAST
THOMAS ULIMWENGU AKISHANGILIA BAO LA PILI LA STARS
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania hapo jana ilishindwa kusonga mbele katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kushiriki katika fainali zijazo za kombe la dunia Brazil baada ya kulazimishwa kipigo cha bao 4-2 kutoka kwa simba wa ivory coast.
Timu zote zilianza pambano kwa kasi kubwa uku kila mmoja akisoma mchezo wa mwenzake lakini katika dakika za mwanzo za mchezo stars walifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia mchezaji wao amri kiemba.
Haikuwachukua muda mrefu Ivory coast kuweza kusawazisha bao hilo kwani katika dakika ya 15 ya mchezo ivory coast walipata bao lao kupitia kwa mchezaji wao lacina traore na kufanya magoli kuwa 1-1.
Katika dakika ya 23 ya mchezo mchezaji Yaya Toure aliweza kuipatia ivory coast bao la pili kufuatia mpira wa adhabu ndogo ambao ulikwenda moja kwa moja nyavuni na kumshinda kipa wa stars Juma kaseja.
Stars walisawazisha bao hilo katika dakika ya 35 kupitia kwa mchezaji wake machachari Thomas Ulimwengu.
Ujanja uliofanywa na mchezaji wa ivory coast Gervinho wa kujidondosha ndani ya eneo la hatari alipokuwa anapambana na Canavaro uliisaidia ivory coast kupata penati katika dakika ya 43 ambayo ilifungwa na Yaya Toure.
Bao la nne la Ivory coast lilipatikana katika dakika ya 88 ya mchezo lililofungwa na Bonny wilfred na kufanya pambano kumalizika kwa matokeo ya bao 4-2.
kwa matokeo hayo ndoto za Tanzania kusonga mbele katika mashindano hayo makubwa zimefikia tamati
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed