Wednesday, November 20, 2013

CRISTIANO RONALDO AFUNGA HAT TRICK NA KUIPELEKA URENO KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014



CRISTIANO RONALDO AKISHANGILIA BAADA YA KUIPATIA URENO BAO LA KWANZA

RONALDO AKISHANGILIA BAO LA KWANZA

IBRAHIMOVIC AKIINAMISHA KICHWA CHINI BAADA YA RONALDO KUFUNGA BAO LA TATU

IBRAHIMOVIC AKIIFUNGIA SWEDEN BAO KWA ADHABU NDOGO

RONALDO NA IBRAHIMOVIC WANAPOKUTANA KATIKA HARAKATI ZAO ZA UWANJANI

WACHEZAJI WA URENO WAKISHANGILIA KUTINGA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI URENO 2014.
MLINZI WA TIMU YA TAIFA YA URENO PEPE AKIMILIKI MPIRA MBELE YA MSHAMBULIAJI WA SWEDEN


Wakicheza ugenini katika uwanja wa Friends Ureno wakiongozwa na Nahodha Cristiano Ronaldo (CR7) wamefanikiwa kutinga katika mashindano ya kombe la dunia yanayotazamiwa kuanza kupigwa mwezi juni 2014 nchini Brazil baada ya hapo jana usikum kuilaza kwa mabao 3-2(Aggr 4-2) timu ya Sweden iliyokuwa ikiongozwa na Nahodha Zlatan Ibrahimovic.

Alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyeweza kuipatia Ureno bao la kuongoza katika dakika ya 50 ya mchezo kabla ya Zlatan Ibrahimovic kusawazisha katika dakika ya 68 na kuongeza bao la pili katika dakika ya 72 na kufanya magoli kuwa 2-1, ilionekana kama Sweden walikuwa wamepania kuizima ureno katika uwanja wa nyumbani lakini katika dakika ya 77 Cristiano Ronaldo tena aliweza kufunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa bao 2-2.

Katika dakika ya 79 Cristiano Ronaldo tena aliwahakikishia Ureno nafasi ya kucheza mashindano hayo ya kombe la dunia kwa kufunga bao la tatu (Hat trick) na kufanya Matokeo ya mchezo huo kuisha kwa mabao 3-2.

Kwa ushindi huo Cristiano Ronaldo ameweza kudhihirisha kwamba yeye ni mchezaji wa kiwango cha juu kabisa duniani na pia ameweza kuwafanya ureno kurudi nchini Brazil kwa mara nyingine tena baada ya kuondoka uko miaka mingi iliyopita baada ya kuitawala nchi hiyo.

VIKOSI

Sweden: Isaksson, Lustig, Nilsson, Antonsson, Martin Olsson, Larsson (Gerndt 90), Elm (Svensson 45), Kallstrom, Kacaniklic (Durmaz 82), Elmander, Ibrahimovic.
Subs not used: Wiland, Jonas Olsson, Granqvist, Wernbloom, Bengtsson, Johansson, Toivonen, Zengin, Nordfeldt.
Booked: Olsson, Antonsson, Kallstrom, Svensson
Goals: Ibrahimovic 68, 72

Portugal: Rui Patricio, Joao Pereira, Pepe, Bruno Alves, Fabio Coentrao (Antunes 52), Meireles (Carvalho 73), Veloso, Joao Moutinho, Nani, Almeida (Ricardo Costa 82), Ronaldo. 
Subs not used: Eduardo, Eder, Bruma, Luis Neto, Ruben Micael, Varela, Josue, Postiga, Beto.
Booked: Nani
Goals: Ronaldo 50, 77, 79

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed