
Carrick akiwa katika harakati zake ndani ya uwanja

Carrick akiwa na mke wake Lisa
Mchezaji wa Manchester United Michael Carrick amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomfanya kuitumikia klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu wa 2015.
Mchezaji huyo kwa sasa yupo nje ya kikosi cha manchester united kutokana na maumivu ya enka ambayo yanamsumbua kwa sasa lakini ameonyesha furaha yake kwa kupata mkataba mpya na klabu hiyo ambayo ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya uingereza (English premier League).
Akiongelea mkataba mpya Carrick Amesema ni furaha kubwa kupata mkataba mpya katika klabu kubwa kama manchester united, nina furaha kucheza katika klabu hii nikiwa chini ya kocha mpya David Moyes.
Nimefanikiwa kushinda mataji makubwa nikiwa na klabu hii na pia natarajia kushinda vitu vingi zaidi nikiwa mahali hapa.
Kocha mkuu wa sasa David moyes ambaye amemfanya Carrick kuwa mhimili mkubwa katika nafasi ya kiungo anafurahishwa na kujitoa kwa mchezaji huyo kwa hali na mali katika kuisaidia klabu hiyo, aliongea maneno hayo akiwa anamsainisha mkataba mpya mchezaji huyo.
Akimwongelea mchezaji huyo kocha david moyes amesema; nimefurahishwa sana kwa michael Carrick kuongeza mkataba mpya .Katika kipindi kifupi nilichokaa hapa haikuwa ngumu kugundua kuwa Carrick ni msomaji mzuri sana wa mchezo na pia ni mtaalamu mzuri sana katika upigaji wa pasi za mwisho.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed