
KURUDI KWA FUNDI: THIERRY HENRY AKIWA MAZOEZINI NA KLABU YA ARSENAL



THIERY HENRY AKIWA NA MCHEZAJI WA UFARANSA EMMANUEL FRIMPONG
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry amerudi katika klabu yake ya zamani ya Arsenal tayari kwa kufanya nayo mazoezi akiwa katika mapumziko ya muda mfupi wakati timu hiyo ikijiandaa na pambano la kesho jumamosi dhidi ya timu ngumu ya Southampton.
Mchezaji huyo yupo kwa mapumziko mafupi ya majira ya baridi katika kipindi hiki ambacho ligi kuu ya nchini marekani maarufu kama MLS imesimama na Timu ya New York Red Bulls ikiwa na wiki nyingi za mapumziko hayo.
Thierry Henry aliichezea kalbu ya Arsenal kwa miaka 8 akipata mafanikio makubwa na klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao 226 katika mashindano yote aliyoshiriki.
Alirudi Arsenal kwa mkopo katika msimu wa 2011/2012 na kuweza kufunga goli moja.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed