Saturday, December 07, 2013

SIJAWAHI KUWA NA MAHUSIANO NA BINTI WA DAVID MOYES

ZAHA AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE UWANJANI
WILFRIED ZAHA AKIKATAA MAHUSIANO YAKE NA BINTI WA MOYES KATIKA MTANDANO WA KIJAMII WA TWITTER
SI KWELI: ZAHA (KULIA) AMEKATAA KUWA NA MAHUSIANO NA BINTI WA MOYES 
LAUREN MOYES (KUSHOTO)

Mchezaji wa Manchester united Wilfried Zaha ameamua kuvunja ukimya katika sakata lake la tuhuma za kimapenzi na binti wa kocha mkuu wa manchester united David Moyes aitwaje Lauren Moyes.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa alitua katika klabu ya Manchester united kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 15 akitokea katika klabu ya Crystal Palace aliponunuliwa na kocha aliyestaafu wa manchester united Sir Alex Ferguson.

Tume ya Habari ya klabu ya Manchester united na mitandao mingi ya kijamii nchini uingereza zimejawa na uvumi kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa siri wa kimapenzi wa mchezaji huyo na binti wa bosi wake David moyes taarifa ambazo mchezaji huyo amezipinga vikali na kuziita ni taarifa za kizushi na za uongo zenye lengo la kumchafua na kumharibia mahusiano yake na kocha wake katika klabu hiyo.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema kwamba kukosekana kwa mchezaji huyo katika kikosi cha manchester united ni kutokana na taarifa za kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi wa mchezaji huyo na binti wa moyes.

Kutokana na taarifa hizo mchezaji huyo amevunja ukimya kwa kutupia posti katika mtandao wa kijamii wa twitter kukanusha kuhusiana na taarifa hizo na uku akisisitiza kwamba kukosekana kwake uwanjani si kwa sababu hizo bali ni kutokana na mipango ya kocha wake na kuendelea kusisitiza kwamba ipo siku atarudi uwanjani wakati muafaka utakapofika.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed