
No 1: CRISTIANO RONALDO AMESHINDA TUZO YA BALLON D'OR NA KUTANGAZWA KUWA MWANASOKA BORA DUNIANI


MACHOZI YA FURAHA: RONALDO ALISHINDWA KUJIZUIA NA KUJIKUTA AKITOKWA NA MACHOZI YA FURAHA BAADA YA KUNYAKUA TUZO HIYO

RONALDO AKIWA NA TUZO YAKE YA MWANASOKA BORA WA DUNIA


AKIWA NA FURAHA: RONALDO AKIWA NA MWANAYE RONALDO JR PAMOJA NA MCHUMBA WAKE IRINA SHAYK
Cristiano Ronaldo ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka 2013 wa FIFA kwa mara ya pili akimshinda mpinzani wake wa siku zote katika tuzo hizo Lionel Messi.
Mchezaji huyo nyota wa klabu ya Real Madrid alipata upinzani mkali kutoka kwa Lionel Messi wa Barcelona na Frank Ribery wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani kuweza kushinda tuzo hiyo kubwa kabisa duniani.
Akiwa na HIsia kali baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo hiyo Cristiano Ronaldo alipanda jukwaani akiwa na mwanaye Cristiano na kutokwa na machozi ya furaha wakati akipokea tuzo yake ya mwanasoka bora wa mwaka wa FIFA.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 sasa ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kufunga magoli 66 katika michezo 56 ya klabu na ile ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya ureno kwa mwaka 2013 na hatimaye kushinda tuzo hiyo ambayo aliipata mara ya mwisho mwaka 2008 akiwa na klabu ya Manchester united.
Pamoja na kutofanikiwa kushinda kombe kubwa kwa mwaka 2013 Ronaldo ameweza kufunga magoli yote manne wakati ureno walipocheza na Sweden na kufanikiwa kushinda na hivyo kuipeleka Ureno katika mashindano ya kombe la dunia nchini ureno mapema mwezi wa sita mwaka 2014.
Akiongea baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Ronaldo uku akitokwa na machozi alisema sina maneno ya kuelezea furaha yangu kwa wakati huu,napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu wa Real madrid kwa mchango wao mkubwa kwangu, Rais wa klabu pamoja na wachezaji wenzangu wa timu ya taifa ya ureno,familia yangu bila kumsahau gwiji wa soka nchini ureno marehemu eusebio mungu amlaze mahali pema peponi.
Wakati huo huo klabu ya Bayern munich imetambulika kama timu iliyovunja rekodi kwa mwaka 2013 kwa kocha wake aliyestaafu Jupp Heynckes kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka 2013 akiwashinda kocha aliyestaafu wa manchester united Sir Alex Ferguson na kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp.
Heynckes aliiongoza Bayern kushinda kombe la ubingwa wa ujerumani Bundesliga, kombe la ujerumani na kuweza kushinda kikombe cha mabingwa barani ulaya (UEFA Champions League) kabla ya kustaafu.
Gwiji wa soka nchini Brazil Pele alitunukiwa tuzo maalumu ya heshima kwa mchango wake alioutoa katika maendeleo ya soka, akiongea baada ya kukabidhiwa tuzo yake pele alisema nimecheza mpira kwa karibia miaka 30 nimeshinda makombe mengi na zawadi nyingi lakini siku zote nilikuwa ninajisikia wivu kuona vijana wa sasa wakishinda tuzo ya Ballon D'or namshukuru mungu hatimaye nimefanikiwa kukamilisha tuzo muhimu sana katika maisha yangu

GWIJI WA SOKA PELE AKIPOKEA TUZO YAKE YA HESHIMA


MACHOZI YA FURAHA BAADA YA KUPOKEA TUZO YA HESHIMA
Timu bora ya FIFA kwa mwaka 2013 imeundwa na wachezaji wafuatao Manuel Neuer , Philipp Lahm, Sergio Ramos, Thiago Silva na Dani Alves katika nafasi ya ulinzi, viungo ni Andres Iniesta, Xavi ana Ribery wakati washambuliaji ni Ronaldo, Zlatan Ibrahimovic na Messi .
Goli bora la mwaka limeenda kwa Ibrahimovic baada ya kufunga goli la umbali mrefu katika pambano la kirafiki dhidi ya uingereza mwezi novemba 2012
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed