Sunday, January 12, 2014

YAYA TOURE ALIVYOTAWAZWA MWANASOKA BORA WA AFRIKA KWA MARA YA TATU



YAYA TOURE AMEPATA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA KWA MARA YA TATU MFULULIZO

YAYA TOURE AKIWA NA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA 2013 WA AFRIKA

CHETI CHA UBINGWA ALICHOKABIDHIWA YAYA TOURE BAADA YA KUSHINDA TUZO

NAFASI YA MSHINDI WA PILI ILIKWENDA KWA KIUNGO WA CHELSEA NA TIMU YA TAIFA YA NIGERIA JOHN OBI MIKEL
Kiungo mahiri wa Manchester city ya uingereza Yaya Habib Toure ametawazwa kuwa mwanasoka bora wa bara la afrika kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alitunukiwa tuzo hiyo katika hafla kubwa iliyofanyika katika jiji la Lagos nchini Nigeria siku ya Alhamisi usiku.

Tuzo hiyo ambayo inatolewa na shirikisho la mpira wa miguu afrika (CAF) inaamuliwa kwa kura zinazopigwa na makocha mbalimbali na wakurugenzi mbalimbali wa ufundi katika bara la afrika.

Yaya Toure ameweza kushinda tuzo hiyo akiwaacha wapinzani wake John Obi Mikel wa Chelsea na Didier Drogba wa klabu ya Galatasaray ambao kwa pamoja walikuwa wakiwania tuzo hiyo.

Yaya Toure mwenye umri wa miaka 30 sasa ambaye amefunga magoli 13 katika michezo 26 aliyoichezea klabu yake ya Manchester city alimaliza msimu uliopita akiwa hana kikombe chochote baada ya kupoteza kikombe cha ligi kuu ya nchini uingereza kwa Manchester city aliweza kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia yanayotazamiwa kuanza kupigwa mwezi wa sita mwaka 2014 nchini Brazil.

Kwa kupata Tuzo hiyo yaya Toure anaungana na Samwel Etoo ambaye aliwahi kuinyakua tuzo hiyo mara tatu mwaka 2003-2005, Didier Drogba alichukua mwaka 2006 na 2009.

Toure pia alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa BBC hapo mwaka 2013.

habari zote kwa hisani ya mtandao wa www.mcfc.co.uk.


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed