
EMMANUEL ADEBAYOR

WAKATI WA FURAHA: MSIMU ULIOPITA ADEBAYOR ALIKUWA NA MAELEWANO MAZURI NA KOCHA VILLA BOAS NA KUWEZA KUISAIDIA VIZURI KLABU YAKE
Ugomvi uliokuwepo kati ya mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji wa klabu ya Tottenham na kocha aliyefukuzwa kazi katika klabu hiyo Andre Villas Boas umebainika kuwa ni kukataa kwa Adebayor kuvua kofia katika mkutano wa klabu hiyo.
Mashabiki wa klabu ya Tottenham walisikitishwa na kitendo cha kocha huyo kutompa nafasi Adebayor katika safu ya ushambuliaji ambayo inalega lega baada ya kuondoka kwa mshambuliaji Gareth Balle.
Mtandao wa maarufu wa dailymail unafichua siri ya ugomvi huo ambao ulikuwa unafukuta kati ya watu hao wawili.
Mwanzoni mwa msimu wa ligi kuu ya nchini uingereza mchezaji Emmanuel adebayor aliingia na kofia katika mkutano wa klabu ya Tottenham kitendo ambacho hakikumfurahisha kocha huyo na hivyo kumwamuru avue kofia yake kitendo ambacho adebayor alikikataa na kurushiana maneno makali na mwalimu huyo kitendo ambacho kilimfanya kocha huyo kumwona Adebayor kama mtovu wa nidhamu na kuamua kutompa nafasi katika kikosi hicho.
Baada ya ugomvi huo kocha Andre Villas Boas aliamua kutomchezesha mchezaji huyo katika pambano lolote isipokuwa katika pambano la kipigo cha aibu cha bao 6-0 kutoka kwa manchester city.
Tangu kufukuzwa kwa kocha AVB Adebayor ameonekana tena uwanjani akiwa na nguvu mpya na kuweza kuisaidia timu yake kufanya vizuri akifunga mabao manne katika michezo mitano ambayo amecheza chini ya kocha mpya Tim Sherwood likiwemo goli moja alilofunga dhidi ya Manchester united hapo juzi.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed