
LUKE SHAW ALIYESIMAMA
Mlinzi wa Timu ya taifa ya uingereza chini ya umri wa miaka 21 na Timu ya Southampton Luke Shaw amezivutia timu mbali mbali za uingereza uku Manchester united chini ya kocha David Moyes na Chelsea inayonolewa na Jose Mourinho zikionyesha nia ya kutaka kumsajili.
Mchezaji huyo ameongea na mwalimu wa klabu ya Southampton na kumweleza nia yake ya kutotaka kuondoka katika klabu hiyo inayotumia uwanja wa St Mary's.
Kutokana na Mchezaji huyo kukataa kuondoka klabuni hapo kuna uwezekano wa Mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo Nicola Cortese kuzikataa ofa zote ambazo zitaelekezwa kwake kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo.
Timu za Manchester united, Chelsea na Arsenal zinapigana vikumbo kuwania saini ya mchezaji huyo anayechezea Timu ya taifa ya uingereza chini ya umri wa miaka 21 ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa ni paundi milioni 20 na ambaye anaonekana kuja kuwa mbadala wa Patrice Evra katika klabu ya Manchester united na mbadala wa Ashley Cole katika klabu ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed