Monday, June 09, 2014

TP MAZEMBE WASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

TP Mazembe yaitandika Zamalek Ligi ya Mabingwa Afrika 

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeishinda klabu ya Zamalek ya Misri kwa bao 1-0 kwenye mechi za makundi ya Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika siku ya Jumapili. Goli pekee la ushindi wa TP Mazembe liliwekwa nyavuni na Mchezaji kutoka Zambia Rainford Kallaba aliyefunga goli pekee lililoipa ushindi TP Mazembe. Kwa matokeo hayo ya Lubumbashi yanamaanisha kwamba Mazembe wanaongoza kundi A wakiwa na pointi sita

Wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club wako nafasi ya pili, wakipitwa kwa alama mbili.

AS Vita walitoka sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Sudan Al Hilal siku ya Ijumaa.

Kwa upande wa kundi B, Entente Setif ya Algeria walibanwa mbavu kwa sare 1-1 nyumbani kwao na Al Ahli Benghazi ya nchini Libya.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed