Wednesday, July 02, 2014

HATUA YA 16 BORA: UBELGIJI 2 -1 USA

KIUNGO WA UBELGIJI KEVIN DE BRUYNE AKIPIGA MPIRA KUWEZA KUIPATIA UBELGIJI
DE BRUYNE AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA UBELGIJI
DE BRUYNE AKIPONGEZWA NA WACHEZAJI WENGINE WA UBELGIJI
ROMELO LUKAKU AKIIFUNGIA UBELGIJI BAO LA PILI
LUKAKU AKIPONGEZWA
KIPA WA MAREKANI TIM HOWARD AKITOKA NJE YA UWANJA KWA HUZUNI BAADA YA KUTOLEWA MASHINDANONI NA UBELGIJI

Magoli ya muda wa nyongeza yaliyofungwa na Kevin de Bruyne na mchezaji wa akiba Romelu Lukaku yaliiwezesha Ubeljiji kuingia hatua ya robo fainali ya kombe la dunia wakati timu hiyo ilipoishinda Marekani magoli 2-1 huko Salvador Brazil.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Ubeljiji kufuzu hatua hiyo ya robo fainali baada ya kipindi cha miaka 28 .

Kipa wa marekani Tim Howard alitajwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo kufuatia mchezo mzuri aliouonyesha kwa kuokoa mikwaju tele kutoka kwa vijana wa Marc Wilmots .

Mshambuliaji chipukizi wa Lille mzaliwa wa Kenya Divock Origi alianza katika mechi hii badala ya Lukaku na alichangia mashambulizi katika lango la Marekani akishirikiana na Jan Vertonghen na De Bruyne.

Hata hivyo kocha Jurgen Klinsmann alilazimika kufanya mabadiliko baada ya Fabian Johnson, kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na DeAndre Yedlin.

Marekani pia walipoteza nafasi nyingi za kushinda mechi hiyo Chris Wondolowski alipopiga nje pasi ya Jermain Jones.

Timu hizo zilishindwa kufungana katika muda wa kawaida na matokeo yakiwa ni 0-0 .

Baada ya kuanza kwa muda wa nyongeza De Bruyne aliunganisha pasi ya Lukaku na kumwacha Howard ameduwaa.

Lukaku aliweza kuihakikishia  ubeljiji tiketi ya robo fainali alipofunga bao la pili katika dakika ya 15 ya kipindi cha ziada na kutokea hapo Ubeljiji wakarejea nyuma kulinda ngome yao.

Labda hatua hiyo haikuwa nzuri sana kwani iliiruhusu Marekani kushambulia lango lao kila walipopata mpira .

Juhudi za vijana wa Klinsmann zilizaa matunda Green alipoweka kimiani pasi ya Michael Bradley na kuipa marekani matumaini ya kufufua kampeni yao .

Marekani iliendeleza  mashambulizi wakitafuta bao la kusawazisha bila mafanikio muda ulikuwa umekwisha na hivyo kujikuta wakiyaaga  mashindano hayo.

Ubeljiji sasa watachuana na Argentina jumamosi ya tarehe 5 julai katika mechi ya Robo fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 28.

Argentina ilijikatia tikiti ya kushiriki robo fainali hiyo baada ya kuilaza Uswisi 1-0.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed