
YAYA TOURE AKIONGEA NA MWAMUZI WA PAMBANO DHIDI YA UGIRIKI BAADA YA UGIRIKI KUPEWA PENATI YA UTATA

GIORGIOS SAMARAS AKIWA CHINI BAADA YA KUCHEZEWA RAFU NA GIOVANI SIO NA HIVYO KUZAWADIWA PENATI ILIYOFUNGWA NA SAMARAS

WACHEZAJI WA IVORY COAST WAKIWA HAWAAMINI BAADA YA KUTOLEWA KATIKA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Manchester City Yaya Toure amevunja ukimya na kuongea kilichopo moyoni mwake kwa kusema hakuna mtu yeyote anayejali kutolewa kwao kwa sababu ni waafrika.
Timu hiyo ya Ivory Coast inayojulikana kwa jina la Utani kama Tembo walitupwa nje ya mashindano ya kombe la dunia katika dakika za majeruhi na ugiriki baada ya Giorgis Samaras kufunga penalti kwa kile kilichodaiwa ni penati ya utata.
Yaya Toure amesisitiza kutolewa kwao kumechukuliwa kama jambo la kawaida na suala kuzimwa kimya, nilitaka mwamuzi aone ujanja uliofanywa na Samaras kuweza kupata penati ile.aliongea Yaya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari nchini ufaransa.
Kwa mara Nyingine tena mwamuzi hakuwa upande wetu. Tulinyimwa Penati zaidi ya moja katika pambano letu dhidi ya Japani na mara hii tena mwamuzi hakuwa upande wetu.
Suala hili halimuumizi mtu yeyote kwa suala hili linawahusu waafrika zaidi na timu zote za afrika.
Nani anajali kuhusu unyanyaswaji wa timu za afrika? kosa lile limetunyima nafasi muhimu sana katika soka la afrika, ni kashfa ambayo kwa bahati mbaya hainyeshi kuumiza mtu yeyote. Timu ya Ivory Coast ilikuwa ndani ya Sekunde 90 za kuweza kuifikia hatua ya 16 bora lakini faulo ya ajabu iliyofanywa na Giovani Sio ilitoa mwanya kwa Samaras kutengeneza penati na kupata ushindi wa bao 2-1
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed