Wednesday, August 20, 2014

LUIS NANI ATUA SPORTING LISBON KWA MKOPO WA MUDA MREFU KUTOKA MANCHESTER UNITED

Winga wa Ureno na Manchester united Luis Nani atimaye ametua katika klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno ambako atakuwa akiitumikia klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja baada ya kuitumika klabu ya Manchester united kwa miaka 7.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 sasa ametua Lisbon ikiwa ni sehemu ya dili kati ya Man united na Klabu ya Sporting Lisbon Kuweza kumwashia mlinzi wake wa kati Marcos Rojo kutua Old traford kwa uhamisho wa paundi milioni 16.

Mchezaji huyo mwenye uraia wa Ureno anarudi kucheza katika ligi ya nyumbani ambayo alikuwa akiichezea kabla ya kutua Manchester united kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 mwaka 2007.
MASHABIKI WA SPORTING LISBON WAKIMPOKEA LUIS NANI 
NANI AKIPOKEA NA WALINZI BAADA YA KUTUA KATIKA JIJI LA LISBON NCHINI URENO
MAPOKEZI YA LUIS NANI NCHINI URENO

Mchezaji huyo alipoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza na hivyo na hivyo kufanikiwa kucheza michezo 13 tu msimu uliopita na kufunga bao moja tu hiyo ikiwa ni katika mashindano ya klabu bingwa brani ulaya dhini ya Bayer 04 Leverkusen.

Nani aliichezea Manchester united pambano la kwanza la msimu huu la kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa swansea alipoingia kuchukua nafasi ya Javier Hernandez.

Kocha mpya wa Manchester united Louis Van Gaal ameona ni bora kumwacha Mchezaji huyo arudi katika klabu yake ya zamani ikiwa ni moja ya jaribio la kuokoa kipaji cha mchezaji nhuyo ambacho kilikuwa shakani kupotea.

Nani anaungana na Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra miongoni mwa wachezaji wenye majina makubwa kuondoka katika klabu ya Manchester united msimu huu wa majira ya joto

REKODI ZA LUIS NANI MANCHESTER UNITED 

Signed: June 2007 for £20million 
2007-08 - Games: 41 Goals: 4
2008-09 - Games: 30 Goals 6
2009-10 - Games 35 Goals 6
2010-11 - Games 49 Goals 10 
2011-12 - Games 40 Goals 10
2012-13 - Games 21 Goals 3
2013-14 - Games 13 Goals 1
2014-15 - Games 1 Goals 0 
Total: Games 230 Goals 40 


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed