Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamekutana hapo jana katika pambano safi la kirafiki kati ya Argentina na Ureno lililopigwa hapo jana katika dimba la Old Trafford na kushuhudia Ureno wakitoka kifua mbele kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Wachezaji hao wawili wenye hadhi ya juu duniani katika mchezo wa soka walikuwa kivutio kikubwa kabla ya pambano hilo lililopigwa katika jiji la Manchester na kushuhudia wachezaji hao wakikumbatiana kabla na baada ya mchezo huo na hivyo kuwafurahisha mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja huo kushuhudia pambano hilo.
Wachezaji hao walicheza pambano hilo la kirafiki lakini hakuna kati yao ambaye aliweza kufunga bao katika pambano hilo uku ikishuhudiwa ureno ikitoka kifua mbele kwa bao safi la dakika ya 90 lilifungwa na Raphael Guerreiro
CRISTIANO RONALDO (KUSHOTO) NA LIONEL MESSI (KULIA)
CRISTIANO RONALDO NA LIONEL MESSI WAKISALIMIANA KABLA YA PAMBANO LA JANA
MESSI NA RONALDO WAKIFURAHI KWA PAMOJA KATIKA PAMBANO HILO
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed