Tuesday, November 18, 2014

MANCHESTER UNITED YAKARIBIA KUMSAJILI KIPA WA ZAMANI WA BARCELONA VICTOR VALDES

Manchester united imeshindwa kumnasa kipa wa zamani wa klabu ya Barcelona Victor Valdes wiki hii ili aweze kuidakia klabu hiyo katika pambano la jumamosi dhidi ya klabu ya Arsenal.

Manchester united imekumbwa na wimbi la majeruhi baada ya Viungo wake wawili Daley Blind na Michael Carick kuumia pamoja na kipa David Degea kurudi katika klabu hiyo kutoka katika mechi za kimataifa akiwa majeruhi.

Degea ambaye ni kipa namba moja wa klabu hiyo amepatwa na maumivu ya kidole na hivyo kutia mashaka katika uwepo wake katika pambano la jumamosi dhidi ya klabu ya Arsenal, ingawa maumivu yake bado hayajathibitishwa kumekuwa na uvumi kwamba kocha mkuu wa klabu ya Manchester united Louis Van Gaal anaweza kumwangalia golikipa namba mbili Anders Lindergaard ili aweze kuiwakilisha klabu hiyo katika pambano la jumamosi na kujitahidi kumtwaa kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdes aweze kuwa kipa wa akiba katika pambano hilo.

KIPA NAMBA MOJA WA MANCHESTER UNITED DAVUID DEGEA AKIONDOKA KATIKA VIWANJA VYA MAZOEZI VYA TIMU YA TAIFA AKIWA MAJERUHI BAADA YA KUUMIA KIDOLE

Valdes anakaribia kupona kabisa na klabu hiyo ipo mbioni kumpa mkataba wa kudumu kuweza kuitumikia na ikizingatiwa kwamba klabu hiyo haijafikisha idadi ya wachezaji 25 ambao ndiyo wanaohitajika katika ligi hiyo. Ingawa maombi ya kumwongeza kipa huyo bado hayajafanyika na inategemewa kuchukua muda mrefu kwa taratibu kukamilika na united bado hawajafanya chochote mpaka wakati huu.Victor Valdes ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Barcelona kumaliza.

GOLIKIPA ANDERS LINDEGAARD (WA PILI KUSHOTO) ANATAZAMIWA KUICHEZEA MANCHESTER UNITED KATIKA PAMBANO LA JUMAMOSI

JUAN MATA AKIMPONGEZA KIPA DAVID KWA KAZI NZURI 

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed