Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kumpatia mkataba mpya kipa wake mahiri David Degea wakati huo huo ikimtambulisha kipa wake mpya namba mbili Victor Valdes ambaye aliwahi kuwa kipa nambari moja wa Klabu ya Barcelona ya Hispania.
United imethibitisha usajili wa Valdes ambaye amepatiwa mkataba wa miezi 18 ukiwa na kifungu kinachomruhusu mchezaji huyo kuongezewa mkataba mpya pindi mkataba wake wa awali utakapomalizika na wakati huo huo kocha mkuu wa manchester united Louis Van Gaal akimtangaza Valdes mwenye miaka 32 kama golikipa namba 2 wa united.
Wakati huo huo katika mustakabali wa baadaye wa kipa David Degea ambaye anakubalika sana na mashabiki wa klabu ya united klabu ina uhakika wa kukubaliana mkataba mpya na kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa.
GOLIKIPA NAMBA MOJA WA MANCHESTER UNITED DAVID DEGEA
KIPA NAMBA MBILI WA MANCHESTER UNITED VICTOR VALDES AKITAMBULISHWA
VICTOR VALDES (KUSHOTO) AKIWA NA KOCHA WA MANCHESTER UNITED LOUIS VAN GAAL
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed