Friday, January 09, 2015

YAYA TOURE ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA KWA MARA YA NNE

Kiungo mchezeshaji wa Klabu ya Manchester City Yaya Toure ametajwa kama mchezaji bora wa mwaka 2014 kwa kuweka rekodi ya kutwaa mara nne mfululizo katika sherehe iliyofanyika katika jiji la Lagos nchini Nigeria hapo jana.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alipata upinzani kutoka kwa Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Gabon Pierre Emerick Aubameyang pamoja na Golikipa mahiri wa Nigeria Vincent Enyeama ili kuweza kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne mfululizo.

Tuzo hiyo ilidhibitishwa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika -CAF kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter hapo jana na kufanya klabu ya Manchester city kutuma salamu za pongezi kwa mchezaji huyo.

YAYA TOURE AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE NDANI YA UWANJA
PIERRE EMERICK AUBAMEYANG (KUSHOTO) NA VINCENT ENYEAMA (KULIA)

Msimu uliopita Yaya Toure alifanikiwa kufunga mabao 24 akiwa na klabu yake ya Manchester City kati ya hayo ishirini yakiwa ni katika Ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu kama EPL na kuiwezesha klabu yake kupata ubingwa kwa mara ya pili katika misimu mitatu.

Katika majira ya joto ya msimu uliopita Yaya Toure hakuwa na mwanzo mzuri katika ligi kuu nchini uingereza  baada ya kumpoteza mdogo wake ibrahimu aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa na pia migogoro iliyojitokeza kati yake na klabu yake ya Manchester city. Sababu hizo zilisababisha kiwango chake kushuka lakini ameweza kupandisha kiwango chake katika muda muafaka ambapo Timu ya taifa ya ivory Coast inajiandaa kwa kombe la mataifa ya Afrika

YAYA TOURE AKIIFUNGIA CITY BAO KATIKA MAPAMBANO YAKE

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed