Friday, July 29, 2016

PAUL POGBA AVUNJA REKODI YA USAJILI BARANI ULAYA ATUA MANCHESTER UNITED KWA ADA YA PAUNDI MILIONI 100



PAUL POGBA AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA UWANJANI NA KLABU YA JUVENTUS YA ITALIA
Paul Pogba anakuwa mchezaji wa Manchester united kwa mara nyingine tena baada ya Manchester united kukubaliana na Juventus ya Italia kumnunua mchezaji huyo kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa paundi milioni 100.

Kukamilika kwa dili hiyo kunamfanya mchezaji huyo ambaye aliondoka manchester united mwaka 2012 kurudi tena klabuni hapo akiwa mchezaji ghali katika ligi ya uingereza huku akivunja rekodi ya usajili nchini humo kwa paundi milioni 40.

Dili ya mchezaji huyo mwenye miaka 23 sasa inategemewa kuhalalishwa leo ijumaa baada ya kuwepo kwa mazungumzo kati ya viongozi wa Juventus na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola pamoja na wanasheria wa mchezaji huyo.

Manchester united na Juventus zote kwa pamoja wamekubaliana kulipa wakala wa mchezaji huyo kiasi cha kiasi cha fedha ambacho ni asilimia 20 ya mauzo ya mchezaji huyo.

Paul Pogba anavunja rekodi ya paundi milioni 86 ambayo iliwekwa na mchezaji Gareth Bale alipotua Real Madrid akitokea Tottenham ya nchini uingereza mwaka 2013.

Mchezaji huyo anatazamiwa kukamilisha taratibu za vipimo vya afya yake katika jiji la Los Angeles katika kipindi hiki ambacho yupo mapumzikoni nchini Marekani kabla ya kusaini dili ya miaka mitano na klabu ya Manchester united ambayo itamfanya aweze kulipwa mshahara wa paundi 290,000 kwa wiki.

Paul Pogba aliondoka Manchester United mwaka 2012 baada ya wakala wa mchezaji huyo kushindwa kukubaliana na kocha wa Manchester united wa wakati huo Sir Allex Ferguson kuhusu kuongezwa kwa Mshahara katika mkataba wake mpya.

Usajili huo unakamilisha idadi ya wachezaji wanne waliosajiliwa na kocha Jose Mourinho baada ya awali kuwasajili mlinzi wa kati Eric Bailly, Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed