
SHWEINSTEIGER AKIPOKEA TUZO YA HESHIMA YA MCHEZAJI BORA WA KUIGWA

HISIA KALI KWA MASHABIKI WA UJERUMANI
SHWEINSTEIGER AKIWA NA KOCHA WA TIMU YA TAIFA JOACHIM LOW

BASTIAN SHWEINSTEIGER AKIONGEA KUWAAGA MASHABIKI WA UJERUMANI

BASTIAN SHWEINSTEIGER AKIWAAGA MASHABIKI WA UJERUMANI WALIOJITOKEZA KUMUAGA
Nahodha wa timu ya taifa ya ujerumani Bastian Shweinsteiger amestaafu rasmi kuichezea timu ya taifa ya ujerumani akiwa na umri wa miaka 32. mchezaji huyo aliaga rasmi katika pambano la kirafiki dhidi ya Finland ambapo ujerumani ilishinda pambano hilo.
Jina la shujaa huyo wa ujerumani lilitajwa mara tatu katika uwanja wa Borussia park kuonyesha shukrani kwa mchango na kujitoa kwa mchezaji huyo katika taifa lake. Akiambatana na rafiki yake wa siku nyingi Lukas Poldoski pamoja na Angel Merkel Shweinsteiger alionekana akiwa mwenye hisia kali kuweza kuwaaga wachezaji wenzake katika hafla ambayo iliandaliwa rasmi kwa ajili ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo aliweza kuzawadiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake alioutoa kwenye timu ya taifa na kuwa mfano wa kuigwa kwa taifa na vizazi vijavyo.
mchezaji huyo ameweza kuichezea timu ya taifa kwa miaka 12 akicheza michezo 121 na kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika kombe la dunia baada ya kuichapa Argentina katika fainali.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed