Sunday, November 25, 2012

WADAU MNALIKUMBUKA BASI HILI?

BASI LA CHELSEA LILIFANYA KAZI NZURI SANA KATIKA MASHINDANO YA KLABU BINGWA BARANI ULAYA MSIMU ULIOPITA LAKINI LIMESHINDWA KABISA KUFANYA MAMBO MAZURI MSIMU HUU

REAL MADRID YAKUBALI KIPIGO CHA BAO 1 KUTOKA KWA REAL BETIS



 Sergio Ramos (Kushoto) na Cristiano Ronaldo (Kulia) wameshindwa kuisogeza mbele real madrid


 Benat Etxebarria (kulia) akifunga goli la pekee

 Ronaldo ameshindwa kufunga katika mechi na Manchester City na Betis
Whack: Jose Maria Callejon and Ronaldo are wiped out by a challenge Jose Maria Callejon na Ronaldo wakiwa katika mpambano
mtu wa kati: Luka Modric ameshindwa kabisa kuisaidia Real

Ronaldo na benzema wakiwa wamechanganyikiwa

Saturday, November 24, 2012

MAPOKEZI YA RAFA BENITEZ


MANCHESTER UNITED 3 QPR 1

Daren Fletcher akishangilia goli la pili la man u
Jammie mark akishangilia goli la QPR
DONDOO LA MECHI
MAN UNITED: Lindegaard; Rafael, Evra, Ferdinand, Evans; Young (Anderson 59), Scholes (Hernandez 59), Fletcher; Rooney, Welbeck (Powell 79), Van Persie Subs not used: De Gea, Jones, Smalling, Cleverley.

Kadi ya njano: Scholes

magoli: Evans 64, Fletcher 68, Hernandez 72.

QPR: Julio Cesar; Traore (Ferdinand 61), Hill, Nelsen, Derry; Taarabt (Hoilett 73), Dyer, Faurlin (Granero 84), M'bia, Cisse, Mackie Subs not used: Green, Diakite, Wright-Phillips, Ephraim.
Kadi ya njano: Mbia.
magoli: Mackie 52.
Attendance: 75,603
Referee: Lee Probert (Wiltshire).

YANGA YASAINI MAKUBALIANO YA UPEMBUZI AKINIFU NA BCEG



Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji kulia akisaini hati ya makubaliano ya upembuzi akinifu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Beijing Construtcion Geng Hijuan



Klabu ya Yanga leo imesaini makubaliano ya upembuzi akinifu na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, juu ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa Kaunda katika eneo la makao makuu ya klabu Jangwani

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa uongozi na kamati ya utendaji na kujadili juu ya hatua hiyo ambayo kampuni ya BCEG itaanza kazi wiki ijayo na pindi itakapokamilisha michoro zoezi litakalofuata itakua awamu ya ujenzi wa uwanja.



Hiki ni kipindi cha kufanya shughuli za kimaendeleo,na hasa kipindi hichi ambacho klabu yetu ipo katika amani na mshikamano kwa viongozi na wanachama, hivyo naamini mara tutakapomaliza suala la uwanja tutaanza pia ujenzi wa jengo lakitega uchumi mtaa wa mafia alisema 'Manji'.

Naye Mkurugenzi wa shirika la BCEG nchini, bwana Geng Hijuan amesema amefurahi kufikia hatua hiyo na klabu ya Young Africans, kazi waliyopewa sasa wataifanya kwa uhakika mzuri na kutoa makadirio halisi juu ya gharama ambazo zitagharimu kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya BCEG kutoka nchini China ndiyo iliyojenga uwanja wa Taifa wa kisasa jijini Dar es salaam na sasa ndio waliopewa kazi ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa Kaunda.

Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amesema, makadirio ya uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji elfu thelathini (30,000) mpaka elfu arobaini (40,000) kutegemea na wataalam watakavyoona, pia utakua na huduma zote za muhimu katika viwanja vya kisasa.

Manji alisema mategemeo ya Kamati ya Utendaji ni kuanza kujengwa kwa uwanja huo mapema kabla ya mwezi juni mwakani, ambapo desemba 8 mwaka huu watasubiria kupata baraka za wanachama katika mkutano mkuu.

Friday, November 23, 2012

SANAMU YA ALEX FERGUSON YAZINDULIWA RASMI LEO OLD TRAFFORD


WACHEZAJI MBALIMBALI WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED WALIHUDHURIA SHEREHE HIYO AKIWEMO MKONGWE WA KLABU HIYO ERICK CANTONA
PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA SANAMU YA ALEX FERGUSON AMBAYO IMEZINDULIWA RASMI LEO KATIKA UWANJA WA OLD TRAFFORD IKIWA NI SANAMU YA HESHIMA KWA KOCHA HUYO AMBAYE AMEIFUNDISHA KLABU HIYO KWA MUDA WA MIAKA 26

BREAKING NEWS...........MARK HUGHES APIGWA PANGA QPR


KOCHA WA ZAMANI WA QPR MARK HUGHES
Mark Hughes amepigwa panga kufundisha klabu ya QPR kufuatia matokeo mabaya katika klabu hiyo, nafasi yake imechukuliwa na Harry Redknapp ambaye ataanza kazi mara moja

Clattenburg hatafunguliwa mashtaka-FA




Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA limetangaza kuwa halitamfungulia mashtaka yoyote refa Mark Clattenburg, ambaye anatuhumiwa kutumia lugha ya ubagusi dhidi ya mchezaji wa Chelsea, wakati wa mchuano wa mechi ya ligi kuu ya premier ya England.

Mcheza kiungo wa Chelsea, Ramires, alidai kuwa alisikia refa huyo akimueleza mchezaji mwingine wa Chelsea John Obi Mikel, Nyamasa nyani huyo wakati wa mechi yao tarehe 28 mwezi uliopita dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge.

Lakini shirikisho hilo limesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha ili kumfungulia mashtakab refa huyo.

WACHEZAJI WA 5 WAWANIA MWANASOKA WA MWAKA WA AFRIKA WA BBC



Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.

Yaya Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.

Mwenzake katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.

Wachezaji wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.

Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata vikombe.

Inaelekea Drogba aliondoka Chelsea wakati muwafaka, mara tu baada ya timu yake kukamilisha msimu kwa ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu, na vile vile akipata bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA.

HABARI KUTOKA TFF



 
Tiketi Za Fainali Za AFCON 2013 Kupatikana Kwa Mtandao 
Washabiki wanaotaka kushuhudia Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini watapata tiketi kwa njia ya mtandao.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tiketi kwa ajili ya washabiki (public tickets) wanaotaka kuhudhuria fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu, zitauzwa kupitia mtandao wa www.afcon2013booking@eqtickets.com . Pia tiketi zitapatikana kupitia simu namba +27 879803000.

Fainali hizo zinazoshirikisha timu 16 zitachezwa Johannesburg, Nelson Mandela Bay, Mbombela, Durban na Rustenburg. Mechi ya fainali itachezwa Februari 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Soccer City jijini Johanesburg kuanzia saa 2 usiku kwa saa za Afrika Kusini.

Mechi ya ufunguzi wa fainali hizo itachezwa Januari 19 mwaka huu ambapo wenyeji Afrika Kusini (Bafana Bafana) wataumana na Cape Verde kuanzia saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Soccer City.

Angola na Morocco zitacheza mechi ya pili kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 3 usiku. Timu zote hizo ni za kundi A. Mabingwa watetezi Zambia wako kundi C na wataanza mechi yao ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Ethiopia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Mbombela. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria na Burkina Faso.

Boniface Wambura
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


U-20 YATINGA ROBO FAINALI, YAICHAPA AYOSSA 5-0



Kikosi cha U-20 cha Young Africans
Kikosi cha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, U-20 cha Young Africans leo kimekata tiketi ya kucheza Robo Fainal ya mashindano ya El Talento Soccer Tournament Cup 2012 baada ya kuichapa timu ya Ayossa FC mabao 5 - 0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Etihad Stadium - Mwananyamala B.

Vijana wa U-20 wa Young Africans wanashiriki mashindano hayo ambayo mshindi ataibuka na zawadi ya tshs Milioni 3, leo walikuwa wanacheza mchezo wa tatu, kufuatia kushinda 2-1 mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Mbagala Market, na sare ya 1-1 dhidi ya Star Rangers

LIVERPOOL 2 YOUNG BOYS 2


TIMU YA LIVERPOOL IMEKOSA NAFASI YA MOJA KWA MOJA KUFUZU KWA HATUA YA MTOANO KATIKA MASHINDANO YA UEFA NDOGO MAARUFU KAMA EUROPA LEAGUE BAADA YA JANA USIKU KULAZIMISHWA SARE YA BAO 2-2 NA YOUNG BOYS NA HIVYO KUIFANYA TIMU HIYO KUSUBIRI PAMBANO LAKE LA MWISHO NA UDINESE ILI WAWEZE KUFUZU KWA HATUA YA MTOANO NA WAKATI HUO HUO WAKISUBIRI MATOKEO YA MWISHO KATI YA YOUNG BOYS NA ANZHI MAKACHKALA

SNOOP DOGGY KUWEKEZA KATIKA KLABU YA CELTIC



MWANAMUZIKI MKONGWE WA HIP HOP SNOOP DOGGY AMBAYE SIKU ZA KARIBUNI AMEJIPA JINA JIPYA LA SNOOP LION AMEFICHUA SIRI YAKE YA MUDA MREFU KWAMBA ANATAKA KUWEKEZA KATIKA SOKA NA YUPO MBIONI KUTOA MAMILIONI YA DOLA KUWEKEZA KATIKA KLABU YA CELTIC YA SCOTLAND

TIMU YA WIKI YA CHAMPIONS LEAGUE



RAFA BENITEZ AANZA KAZI RASMI CHELSEA


KOCHA MPYA WA CHELSEA RAFA BENITEZ AKIWA KATIKA JEZI YA KLABU YAKE MPYA YA CHELSEA
RAFA BENITEZ AKIWA MAZOEZINI NA KLABU YA CHELSEAKOCHA MPYA WA CHELSEA RAFA BENITEZ AMEPOKELEWA RASMI KATIKA KLABU YA CHELSEA NA KUKABIDHIWA MAJUKUMU ALIYOYAACHA MUITALIANO ROBERTO DI MATTEO KATIKA KUINOA TIMU HIYO YA DARAJANI, KOCHA HUYO AMEONEKANA KWA MARA YA KWANZA KATIKA MAZOEZI YA KLABU HIYO HAPO JANA.

Thursday, November 22, 2012

NIGERIA KUZAWADIWA DOLA 90,000 KILA MMOJA KAMA WAKISHINDA AFRICAN CUP OF NATION MWAKANI


CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU NCHINI NIGERIA(NFF) KIMETOA AHADI YA FEDHA DOLA 90,000 KWA KILA MCHEZAJI WA NIGERIA ENDAPO TIMU HIYO YA TAIFA ITAFANIKIWA KUCHUKUA UBINGWA WA AFRIKA HAPO MWAKANI MASHINDANO YATAKAYOFANYIKA NCHINI AFRIKA YA KUSINI KUANZIA JANUARI 2013.

MSEMAJI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU NCHINI HUMO ADEMOLA OLAJIRE AMETHIBITISHA KWAMBA WACHEZAJI HAO WATAKUWA WAKIPATA DOLA 10,000 KILA MMOJA WAKIFANIKIWA KUFUNGA KATIKA KILA MECHI KATIKA HATUA ZA MAKUNDI,DOLA 15,000 KILA MMOJA WAKIFANIKIWA KUINGIA ROBO FAINALI, DOLA 20,000 NYINGINE WAKIFANIKIWA KUTINGA NUSU FAINALI NA DOLA 25,000 WAKIFANIKIWA KUINGIA FAINALI.
 
KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO HILO BWANA MUSA ADAMU SAIDI AMESEMA LENGO LA MKAKATI HUO NI KUWATIA HAMASA WACHEZAJI ILI WAWEZE KUFANYA VIZURI KATIKA MASHINDANO HAYO NA KUILETEA NCHI YA NIGERIA HESHIMA.

DIDIER DROGBA KUTUA CHELSEA KWA MUDA MFUPI



 
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba ambaye anakipiga katika klabu ya Shanghai Shenhua ya China ameliomba ruhusa shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA kumpa ruhusa ya kuweza kujiunga kwa muda na timu yake ya Zamani ya Chelsea kwa kipindi kifupi wakati ligi ya nchini china ikiwa katika mapumziko.

Mchezaji huyo ambaye anajiandaa kuitumikia Timu yake ya taifa ya Ivory coast katika Mashindano makubwa ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mapema mwezi januari 2013 nchini afrika ya kusini ataitumia nafasi hiyo kama sehemu ya maandalizi yake binafsi kabla timu ya taifa ya ivory coast haijaanza rasmi maandalizi yake kuelekea afrika ya kusini.

Kama FIFA itamruhusu Drogba kuichezea chelsea katika mashindano yake itakuwa imepingana na sheria yake inayomtaka mchezaji kutoichezea timu nyingine kabla ya Dirisha dogo la usajili la Januari halijafunguliwa.FIFA imeshawahi kukataa maombi kama hayo kutoka kwa wachezaji mbalimbali wakiwemo David Beckham, Thiery Henry na London Donovan

RAFA BENITEZ AKAMATA MIKOBA ILIYOACHWA NA ROBERTO DI MATTEO


 
KOCHA WA ZAMANI WA LIVERPOOL RAFA BENITEZ YUPO MBIONI KUTUA CHELSEA KUKAMATA MIKOBA ILIYOACHWA WAZI NA KOCHA ROBERTO DI MATTEO AMBAYE KIBARUA CHAKE KATIKA KUITUMIKIA KLABU HIYO YA DARAJANI KILIFIKIA TAMATA JUZI SIKU YA JUMANNE BAADA YA HARAKATI ZAKE ZA KUTAKA KUTETEA UBINGWA WA ULAYA KUGONGA MWAMBA KWA KUKUBALI KIPIGO CHA BAO 3-0 KUTOKA KWA KLABU YA JUVENTUS YA ITALIA NA HIVYO KUWEKA REKODI YA KUWA BINGWA WA KWANZA MTETEZI WA KOMBE HILO KUONDOLEWA MAPEMA KATIKA HATUA ZA MAKUNDI.

MANCHESTER CITY 1 REAL MADRID 1 MANCHESTER CITY YAONDOSHWA KATIKA KLABU BINGWA BARANI ULAYA

Wednesday, November 21, 2012

BREAKING NEWS: ROBERTO DI MATEO ATIMULIWA CHELSEA


KOCHA WA ZAMANI WA KLABU YA CHELSEA ROBERTO DI MATEO AMETIMULIWA LEO KUIFUNDISHA TIMU HIYO KUTOKANA NA MLOLONGO WA MATOKEO MABOVU YALIYOIKUMBA KLABU  KLABU HIYO KATIKA SIKU ZA KARIBUNI.

Sunday, November 18, 2012

SERENGETI BOYS YAITOA NISHAI CONGO BRAZZAVILLE KWA KUIFUNGA 1-0


Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0. (Picha zote na Habari Mseto Blog)


Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya mchezo kumalizika.

  Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mchezo huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys imeshinda 1-0.

Mshambuliaji wa timu ya Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni mwake.

MAGOLI YA ARSENAL


MSIKOSE KUJA KUTOA SAPOTI


U-20 YANGA 1 - 1 STAR RANGERS


Kikosi cha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, U-20 cha Young Africans leo kimetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Stars Rangers ya Kimara katika mchezo wa makundi wa mashindano ya El Talento Soccer Tournament Cup, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Etihad Stadium - Mwananyamala B.

Vijana wa U-20 wa Young Africans wanashiriki mashindano hayo ambayo mshindi ataibuka na zawadi ya tshs Milioni 3, leo walikuwa wanacheza mchezo wa pili, kufuatia kushinda 2-1 mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Mbagala Market.

Stars Rangers walionekana kukakamia mchezo huo, ukizingatia timu ya U-20 Yanga tangu mwezi wa saba (julai) imeshacheza jumla ya michezo 23, ikishinda michezo 18, sare 4 na kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa utangulizi wa ligi kuu ya Vodacom.

THIERY HENRY NA SOUL CAMPBEL WAISHUHUDIA ARSENAL IKIIUA TOTTENHAM

KOCHA MKUU WA ARSENAL ARSENE WENGER AKIMKARIBISHA MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL THIERY HENRY
WAKIONYESHA MAPENZI YAO YA DHATI KWA KLABU YAO YA ZAMANI SOUL CAMPBEL (KATIKATI) AKIWA NA THIERY HENRY WALIPOKUWA WAKIANGALIA PAMBANO KATI YA ARSENAL NA TOTTENHAM AMBAPO ARSENAL WALIIBUKA NA USHINDI MNONO WA BAO 5-2